Ufafanuzi matukio ya 'kustaajabisha' mchezo wa Simba dhidi ya Lipuli Fc

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Nov 2018
Ufafanuzi matukio ya 'kustaajabisha' mchezo wa Simba dhidi ya Lipuli Fc
Kile kilichodaiwa ni ushirikina baina ya wachezaji wa Simba na Lipuli, katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa jana Ijumaa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kimefafanuliwa na wachezaji ambao wamefanya tukio hilo waliodai mchezo huo una vitu vizito tofauti na wanavyotazamwa na mashabiki wao.

Alianza kiungo wa Simba, Hassan Dilunga kugoma kutoka uwanjani baada ya kumalizika dakika 45 za mwanzo, alikuwa anamsubiri Ibrahim Job wa Lipuli atoke kwanza kisha yeye awe wa mwisho, kitu hicho kiliwastaajabisha mashabiki wengi.

Kipindi cha pili kipa wa Lipuli, Mohamed Ally na Miraji Athuman waliingia uwanjani kupitia sehemu ya kibendera.

Vituko hivyo vilizidi kuleta tafsiri ya aina yake katika mechi hiyo, iliyoisha kwa suluhu.

Mlinda lango wa Lipuli Fc Ally ambaye ni miongoni mwa waliohusika katika matukio hayo alisema hayo yalikuwa masuala ya imani tu.

"Kwenye mpira kuna vitu vizito, pengine kuliko unavyodhani kwa kutazama mpira unavyochezwa.

"Hizo ni imani za mtu husika unayemuona anafanya hivyo, ingawa mwisho wa picha soka ni uwanjani na dakika 90 lazima zitatoa mavuno kwa kila aliyecheza, mavuno yetu leo ni kuambulia pointi moja dhidi ya Simba,"alisema.

Kwa upande wa Athuman alitoa sababu ya kuingilia kwenye kibendera kuwa ilikuwa mbinu ya kuwatoa mchezoni wachezaji wa Simba kuhakikisha wanapunguza kasi ya mashambulizi.

"Unajua mpinzani anapoanza kukufanyia vituko, wewe fanya zaidi yake hapo ndipo unapommaliza mpinzani wako, nimeona mbinu zetu zimefanikiwa kupata suluhu uganini na timu kama Simba si jambo dogo,"alisema.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
23h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’