Baada ya mapumziko ya wiki mbili kupisha michuano ya Kimataifa iliyo kwenye kalenda za CAF na FIFA, ligi kuu ya Tanzania Bara inaendelea kesho Alhamisi Novemba 22 kwa michezo ya kiporo kupigwa.
Kulingana na ratiba iliyotolewa na TFF, kesho kutakuwa na michezo miwili ambapo Yanga itaanza 'kuonja' machungu ya michezo ya mikoani ambapo itakuwa mkoani Shinyanga kuumana na Mwadui Fc.
Nao vinara wa ligi hiyo Azam Fc watakuwa uwanja wao wa nyumbani, Azam Complex kupepetana na Ruvu Shooting.
Mabingwa watetezi, Simba wao watashuka uwanja wa Taifa keshokutwa Ijumaa kuikabili Lipuli Fc.
Hii hapa ratiba ya michezo yote inayopigwa wikiendi hii ambayo itarushwa mbashara na Azam TV;

ADVERTISE HERE