Simba bado haijatangaza usajili wakati huu wa dirisha dogo la usajili lililofunguliwa wiki iliyopita na likitarajiwa kufungwa mwezi ujao, Disemba 15.
Licha ya ukimya huo, taarifa za uhakika kutoka ndani ya uongozi wa mabingwa hao wa Tanzania Bara ni kuwa watasajili ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chao.
Usajili huo utakuwa unalenga zaidi kwenye ligi na mashindano ya ndani kwani dirisha la usajili wa CAF tayari limefungwa na litafunguliwa tena mwanzoni mwa mwaka 2019 kabla ya kuanza kwa hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho.
Hata hivyo uongozi wa Simba bado haujafanya maamuzi kwa kuwa bado haujapokea ripoti kutoka kwa Aussems.
Hivi karibuni Aussems alinukuliwa na vyombo vya habari akisema alikuwa na mpango wa kusajili wachezaji wawili tu lakini upo uwezekano wa idadi hiyo kuongezeka kufuatia kuumia kwa beki Shomari Kapombe ambaye atakuwa nje kwa muda mrefu.
Aussems anatarajiwa kukutana na uongozi wa Simba wakati wowote ambapo pamoja na mambo mengine, anatarajiwa kutoa maoni yake kuhusu usajili.

ADVERTISE HERE