Amunike ajitetea baada ya kipigo cha Lesotho

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Nov 2018
Amunike ajitetea baada ya kipigo cha Lesotho
Baada ya kushushiwa lawama mashabiki kwa kikosi alichopanga kwenye mchezo wa jana, kocha Mkuu wa Taifa Stars Emmanuel Amunike amesema uamuzi wake ulitokana na mwenendo wa wachezaji mazoezini.

Jana Stars ilichapwa bao 1-0 na Lesotho katika mchezo ambao Stars ilihitaji ushindi ili iweze kufuzu kwa fainali za AFCON 2019

Amunike amesema baadhi ya wachezaji hawako katika viwango bora kama wanavyodhani mashabiki.

"Tumefanya mazoezi Afrika Kusini kwa siku 10. Nimepata muda wa kuwatathmini wachezaji wote. Lakini siwezi kutoa maelezo ya ndani zaidi kuhusu wachezaji," amesema

"Nawapanga wale waliotayari kujitoa kwa ajili ya timu. Bahati mbaya wengine hawako katika ubora wao.

"Sina nia ya kumkosoa mchezaji yeyote. Sina tatizo na John Bocco wala Mkude, tufahamu hii ni timu ya Taifa na sio Simba"

Kocha huyo pia ameomba radhi kwa matokeo hayo ambayo hata hivyo amesema yabidi kuyakubali kwani ni sehemu ya mchezo.

Amesema Stars bado ina nafasi ya kufuzu hivyo watajipanga kuhakikisha wanatumia nafasi hiyo kwenye mchezo dhidi ya Uganda utakaopigwa mwakani
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
2h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
20h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’