Watanzania leo walikuwa na matumani makubwa kuwa pengine huu ndio mwaka ambao tumepata nafasi ya wazi kuweza kutinga fainali za AFCON baada ya kusubiri kwa miaka 38.
Hata hivyo kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Lesotho kinaweza kuwa kimefifisha matumaini ya kufuzu kwani Stars inahitaji kushinda dhidi ya Uganda ambayo tayari imefuzu bila ya kupoteza mchezo wala kuruhusu hata bao moja!
Wakati huo huo itabidi kuiombea mabaya Lesotho ifungwe na Cape Verde kwenye mchezo wake wa mwisho utakaopigwa huko Cape Verde.
Kocha Mkuu wa Stars Emmanuel Amunike amelaumiwa kutokana na kikosi alichopanga kwenye mchezo huo.
Siku ambayo Stars ilihitaji ushindi, Amunike amepanga kikosi ambacho kilikuwa na nafasi ndogo sana ya kuipa Stars ushindi.
Uamuzi wake wa kuwaacha nje wachezaji wazoefu huku akiwabadilishia wengine majukumu umelalamikiwa na wengi.
Baadhi ya wachezaji kama Gadiel Michael kwa asili ni mlinzi wa pembeni hivyo kumtumia kama winga hakukuwa na faida yoyote.
Hali ilikuwa hivyo kwa Himid Mao ambaye alipangwa kucheza namba saba wakati nje alikuwepo Shiza Kichuya ambaye alipoingia alibadili sura ya mchezo.
Pia kuwaweka nje wachezaji wazoefu kama John Bocco, Thomas Ulimwengu kunatajwa kuwa sababu nyingine ambayo imeiangusha Stars leo.
Amunike alitumia mfumo wa kujihami zaidi ambao haukufaa katika mchezo ambao Stars ilihitaji kushinda.

ADVERTISE HERE