Stars inaweza kufuzu leo, tuwe watulivu - Amunike

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Nov 2018
Stars inaweza kufuzu leo, tuwe watulivu - Amunike
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo saa 11 jioni kwa saa za Tanzania kitakuwa Maseru kuikabili Lesotho katika mchezo muhimu ambao matokeo yake huenda yakaandika historia kwa soka la Tanzania.

Kama Stars itashinda leo basi itakata tiketi ya kutinga fainali za Michuano ya AFCON itakayofanyika nchini Cameroon mwakani mwezi wa sita.

Hiyo itakuwa mara ya pili kwa Stars kufuzu kwenye michuano hiyo ambayo ilifuzu kwa mara ya mwisho miaka 38 iliyopita

Kocha Mkuu wa Stars Emmanuel Amunike amesema wamefanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo huo na wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri.

Hata hivyo ametahadharisha shamrashamra zisianze mapema hadi baada ya dakika 90 za mchezo huo.

Amunike amesema wanatambua mchezo huo hautakuwa mwepesi kwani Lesotho ni timu nzuri na pia itakuwa inacheza kwenye dimba lake la nyumbani.

Pia timu hiyo nayo itafufua matumaini ya kufuzu fainali za michuano hiyo kama itashinda mchezo huo.

"Michuano ya AFCON mwaka huu imeonyesha utofauti mkubwa. Timu ambazo zilikuwa hazipewi nafasi zimeweza kufuzu mapema. Nasi kesho tunaweza kuwa miongoni mwa timu hizo kama tutashinda"

"Lakini ni vyema tukawa watulivu. Ni rahisi kuwaambia watu utafanya hivi au vile lakini mpira hauko hivyo. Matokeo ni lazima yapatikane uwanjani," amesema Amunike

Jana jioni kikosi cha Stars kilifanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo huo ambao wachezaji watatu wataukosa kutokana na sababu mbalimbali.

Nahodha Mbwana Samatta atakosekana kwa kuwa anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano wakati Shomari Kapombe na Rashindi Mandawa wao ni majeruhi.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
6h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
7h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
10h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’