Aliyekuwa kocha wa Gor Mahia Dylan Kerr ameachana na klabu hiyo jana baada ya kuuandikia uongozi wa timu hiyo barua ya kujiuzulu nafasi yake.
Jana jioni uongozi wa Gor Mahia ulithibitisha kuachana na Kerr aliyeisaidia kutwaa taji la 16 na 17 ligi kuu ya Kenya.
Uamuzi huo wa Kerr umewastua mashabiki wa Gor Mahia kwani kocha huyo wa zamani wa Simba aliweza kuifanya timu hiyo kuwa miongoni mwa timu za kuogopwa Afrika Mashariki na Kati.
Msimu uliopita Kerr aliisaidia Gor Mahia kutinga hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo ilipangwa kundi moja na Yanga.
Kwenye michuano hiyo Kerr aliiongoza Gor Mahia kuifumua Yanga mabao 4-0 huko Kenya na 3-2 hapa jijini Dar es salaam.
Kocha huyo amedai kuwa amepata timu nyingine.

ADVERTISE HERE