Aussems kuwatumia Big Bullets kutathmini kikosi leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
16 Nov 2018
Aussems kuwatumia Big Bullets kutathmini kikosi leo
Kocha wa Simba, Patrick Aussems, amesema kuwa mchezo wa leo wa kirafiki dhidi ya Big Bullets ni kipimo kizuri kwa timu yake kuelekea kwenye mchezo wao wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swallows wa Swaziland.

Aussems, amesema kuwa kama kocha kiu yake ni kuona Simba inafanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa na ndio ndoto ya viongozi wa timu hiyo.

Amesema kuwa mchezo wa leo dhidi ya Wamalawi hao ni kwa ajili ya kuangalia upungufu mdogo mdogo kwenye kikosi chake ili aweze kuyafanyia kazi mapema kabla ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Niliuomba huu mchezo maalum kuwapima wachezaji wangu, tunajiandaa kucheza mchezo muhimu wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kipimo kama hiki ni muhimu sana na kitatusaidia kuona nini tunapaswa kuongeza,” alisema Aussems.

Aidha, alisema kuwa alitamani kama wachezaji wake wote wangekuwapo kwenye mchezo wa leo, lakini majukumu ya timu za taifa ni muhimu.

“Tutacheza kwa umuhimu mchezo huu, Big Bullets ni timu kubwa na nzuri itatupa kipimo kizuri kwetu, wachezaji wangu nataka wanionyeshe kile tunachokifanya mazoezini,” alisema Aussems.

Amesema baada ya mchezo wa leo, pia atahitaji mchezo mwingine wa pili kabla ya kuvaana na Mbabane Swallows kwenye mchezo wao wa kwanza.

“Viongozi wameniambia wanafuatilia mchezo mwingine na timu itakapopatikana tutacheza nao, michezo hii ya kirafiki ni muhimu kuelekea kwenye michuano ya kimataifa,” alisema Aussems.

Mchezo huo wa leo unatarajiwa kuanza majira ya saa 12:00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
13h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
19h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
21h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →