Juma Luizio atafuta njia ya kutokea Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Nov 2017
Juma Luizio atafuta njia ya kutokea Simba
Mshambuliaji Juma Luizio alikuja Simba msimu uliopita kwa mkopo akitokea ZESCO ya Zambia kabla hajasajiliwa kwa mkataba wa mwaka mmoja mwezi Julai.

Licha ya kupewa nafasi mara kadhaa Luizio ameshindwa kulishawishi benchi la Ufundi la Simba hivyo kupelekea nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza kuwa finyu.

Kuna taarifa kuwa Singida United inamnyemelea mshambuliaji huyo na kocha Hans van Pluijm ameahidi kumfanya miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha kwanza.

Luizio amesema atazungumza na uongozi wa Simba kuona uwezekano wa kuvunja mkataba wake kwani hayuko tayari kutolewa kwa mkopo.

Simba inakusudia kuimarisha safu yake ya ushambuliaji wakati huu wa dirisha dogo la usajili hivyo italazimika kuwaondoa baadhi ya wachezaji iwe kwa mkopo au kuwauza.

Mchezaji mwingine aliye hatarini kuuzwa ni mshambuliaji Laudirt Mavugo anayehusishwa na klabu ya Gor Mahia, mabingwa wa Kenya.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
13h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
19h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
21h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’