Wachezaji Simba kuingia kambini kesho

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Nov 2018
Wachezaji Simba kuingia kambini kesho
Kikosi cha Simba licha ya kuwakosa nyota wao wengi waliokuwa katika timu zao za Taifa, kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterans.

Baada ya mazoezi ya kesho Alhamisi asubuhi, wachezaji wa Simba wataingia kambini katika Hoteli ya Sea Scape kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Big Bullets ya Malawi.

Kocha wa Simba Patrick Aussems amesema wanaendelea na mazoezi ili kila mchezaji aweze kuwepo katika kiwango bora na ufiti ule ule.

"Waliokuwa katika kambi ya timu ya Taifa wanafanya mazoezi na ndio maana waliobaki hapa nao wanafanya ili kulingana nao na watakapo kuwa pamoja kazi inakuwa ile ile kama hapo awali," alisema.

Simba wiki iliyopita walifanya mazoezi ya nguvu ndani ya Gym viwanja vya Gymkhana na walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya vijana ya Azam ambao waliwafunga bao 1-0 lililofungwa na Said Ndemla.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’