Mbabane Swallows 'yaigwaya' Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Nov 2018
Mbabane Swallows 'yaigwaya' Simba
Baada ya kupangwa kuanza na mabingwa wa Tanzania Bara, Simba kwenye mchezo wa hatua ya awali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Mbabane Swallows imeonyesha 'mchecheto' kuelekea mchezo huo.

Ujumbe ulioandikwa kwenye ukurasa wa mtandao wa Facebook wa timu hiyo unaonyesha kuihofia Simba hasa baada ya kubaini ina wachezaji 10 wanaocheza timu za Taifa

"Tumepangwa na timu kutoka nchini Tanzania, Simba kwenye mchezo wa awali wa michuano ya ligi ya mabingwa," umesema ujumbe huo.

"Sio ratiba mbaya na lengo letu ni kama msimu uliopita, kufuzu kwa hatua ya makundi"

"Hata hivyo Simba sio timu ya kubeza, ina wachezaji nane kwenye timu ya Taifa. Wanacheza mchezo mzuri na ina washambuliaji wa pembeni wenye kasi"

Mbabane Swallows inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Swaziland, itakuja nchini kati ya Novemba 27-28 kuivaa Simba kwenye uwanja wa Taifa kabla ya mchezo wa marudiano wiki moja baadae huko Uswazi.

Simba inaendelea na maandalizi kuelekea mchezo huo ambapo Ijumaa wiki hii itacheza na mabingwa wa Malawi, Big Bullets kwenye mchezo wa Kimataifa wa kirafiki.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
5h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
11h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
14h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’