Mabingwa watetezi Simba wanajiandaa kucheza mechi ya kwanza ya kimataifa ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swallows ya Swaziland na ili kujiweka fiti kabla ya mechi hiyo, watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Malawi, Big Bullets siku ya Ijumaa.
Simba itaanzia nyumbani kati ya Novemba 27 hadi 29 na mechi ya marudiano itakuwa Desemba mwanzoni wakati Big Bullets ambao ni mabingwa mara 12 kwenye ligi ya kwao watakwenda Nairobi kucheza na Gor Mahia.
Kocha wa Simba, Patrick Aussems ameomba kucheza mechi mbili za kimataifa za maana ambazo anaamini zitakuwa kipimo sahihi kwake kabla ya kuvaana na Mbabane ili kuona mapungufu na ubora wa kikosi.
Uongozi wa Simba haraka ulitii uamuzi huo kwa kutafuta timu ambazo zitaipa ushindani Simba na walifanikiwa kuipata Big Bullets na Aussems atatesti mitambo yake Ijumaa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi nyingine ambayo Simba wameomba kucheza ni dhidi ya Al Hilal ya Sudan lakini imeelezwa haina uhakika sana wa timu hiyo kucheza na Simba kwani siku ambayo walikubali kucheza mechi hiyo Simba watakuwa katika maandalizi makali ya kuwakabili Mbabane.
Mratibu wa Simba, Abbas Selemani alisema kocha aliomba mechi hizo za kirafiki zenye ushindani mkubwa ili azitumie kurekebisha kikosi chake kabla ya mechi yao na Mbabane.
“Tulifanikiwa kuwapata Big Bullets na watakuja kucheza hapa, Al Hilal tulikubaliana nao lakini sidhani kama tutacheza nao kwa sababu walitaka uchezwe kati ya Novemba 25-27 siku ambazo tutakuwa katika maandalizi ya kucheza na Mbabane.
“Wachezaji watakaotumika katika mechi hiyo ya kirafiki ni wale ambao watakuwa kambini na si wale waliokuwa kwenye majukumu ya timu zao za Taifa,” alisema Selemani.
Kwa upande wa Aussems alisema, “Wiki iliyopita tulicheza mechi na timu ya vijana ya Azam ambayo kwangu haikuwa mechi kwani niliona kama mazoezi tu, lakini hii na Big Bullets itakuwa kipimo sahihi kulingana na mazoezi ambayo tunafanya.”
“Yote hayo ni maandalizi ya kuona jinsi gani tunafikia malengo ya kufanya vizuri katika mechi za kimataifa na mashindano mengine ingawa baadhi ya wachezaji wapo timu zao za Taifa lakini naamini mambo yanazidi kwenda vizuri kuliangana na mazoezi ambayo tunafanya,” Aussems amenukuliwa na Mwanaspoti.

ADVERTISE HERE