Hesabu kali za Aussems kuelekea mechi dhidi ya Mbabane Swallows

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Nov 2018
Hesabu kali za Aussems kuelekea mechi dhidi ya Mbabane Swallows
Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems, ametaja mkakati wake wa maandalizi utakaomwezesha kuibuka na ushindi dhidi ya Mbabane Swallows ya Swaziland na kisha kufika mbali zaidi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Simba imepangwa kucheza na Mbabane Swallows ambapo itaanzia nyumbani Uwanja wa Taifa Novemba 27, mwaka huu kabla ya kurudiana ugenini baada ya wiki moja.

Aussems amesema tayari wameshaanza mkakati kuelekea kwenye mchezo huo na anataka kuona kasi yao inahamia kwenye michuano hiyo.

Alisema tayari ameomba kutafutiwa mikanda ya video ya wapinzani wao hao ili kuwasoma na kujua nini wafanye kuelekea kwenye mchezo wao huo.

β€œMoja ya mikakati yetu kwanza pamoja na kuwa tunataka kutetea ubingwa wetu wa Ligi Kuu, lakini pia tunataka kufanya vizuri kwenye mashindano ya CAF..., kiufundi tayari nimeanza mikakati ya kujiandaa na mchezo wetu wa kwanza,” Aussems amenukuliwa na gazeti la Nipashe

Alisema wana kikosi imara cha kuweza kufanya vizuri, lakini pia anafikiria kuongeza wachezaji wengine kukiimarisha zaidi.

β€œBado tuna nafasi ya kuongeza wachezaji, nataka kuwa na kikosi imara zaidi kitakachotuwezesha kufanya vizuri Afrika, sitaki kuona tunaishia hatua za mwanzoni kwenye michuano hii ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema Aussems.

Kocha huyo anaendelea na programu yake ya mazoezi ambapo wanafanya mara mbili kwa siku kwenye Uwanja wa Boko Veteran wakati huu wa mapumziko ya kupisha ratiba ya mechi za kimataifa.

Simba inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 26 baada ya kucheza michezo 11 ikizidiwa kwa pointi nne na vinara wa Azam FC ambao wapo mbele mchezo mmoja.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
9h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
15h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’