Ulimwengu akiri, yuko kwenye mazungumzo na Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Nov 2018
Ulimwengu akiri, yuko kwenye mazungumzo na Simba
Mshambuliaji wa zamani wa TP Mazembe Thomas Ulimwengu amekiri kuwepo mazungumzo baina yake na klabu ya Simba iliyoonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Ulimwengu ambaye hivi karibuni alivunja mkataba katika klabu ya El Hilal aliyoitumikia kwa miezi minne pekee, kwa sasa ni mchezaji huru.

Kuna taarifa kuwa Simba inataka kumuongeza kwenye kikosi chake kilichopania kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabaingwa barani Afrika inayoanza mwishoni mwa mwezi huu.

Ulimwengu anao uzoefu mkubwa wa soka la Afrika kwani alifanikiwa kutwaa taji hilo wakati akiitumikia TP Mazembe misimu mitatu iliyopita.

"Yapo mazungumzo lakini hayajafikia kiwango cha kuweza kuyazungumza katika vyombo vya habari," amesema Ulimwengu baada ya kuulizwa kama anaweza kutua Msimbazi

Kwa sasa Ulimwengu yuko nchini Afrika Kusini na kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars' kinachojiandaa kuikabili Lesotho katika mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’