Aussems apania kuunda kikosi cha maangamizi ligi ya mabingwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
9 Nov 2018
Aussems apania kuunda kikosi cha maangamizi ligi ya mabingwa
Wakati nyota ya mshambuliaji Emmanuel Okwi ikizidi kung’aa kwa kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi ligi kuu kwa mwezi Oktoba, Kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema anafikiria kuongeza nyota wengine kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya mashindano ya kimataifa.

TFF jana ilimtangaza Okwi kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba baada ya kuwashinda wapinzani wake Yahya Zayd na Eliud Ambokile waliofika fainali.

Aussems alisema kuwa licha ya timu yake kufanya vizuri kwenye ligi, bado matamanio yake ni kuwa na kikosi imara zaidi kitakachoweza kupambana kwenye mashindano ya kimataifa.

“Kikosi nilichonacho sasa ni imara na kizuri, tunaweza kupambana na timu yoyote, lakini nataka kuongeza wachezaji wengine kuiimarisha zaidi timu,” alisema Aussems.

Aidha, bila kutaja wachezaji gani anaotaka kuwasajili na kwenye nafasi gani, Aussems alisema ana nafasi nne kwa ajili ya wachezaji wa kimataifa na atazitumia.

Simba inajiandaa na mchezo wake wa kwanza wa hatua ya kwanza ya ligi yamabingwa Afrika ambapo wamepangwa kucheza na Le Messenger FC Ngozi ya Burundi kati ya Novemba 27 na 28.

Mabingwa hao wa Tanzania tayari wameshatuma majina ya wachezaji hao kwa Shirikisho la soka Afrika (CAF) huku wakiliengua jina la Nicolaus Gyan kutoka Ghana.

Kuondolewa kwa Gyan kunafanya Simba kuwa na nafasi nne ya kuongeza wachezaji wa kimataifa.

Dirisha dogo la usajili nchini litafunguliwa Novemba 15 na kufungwa Desemba 15

Nipashe
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
10m ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE →
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
17h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
20h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
21h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
23h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →