Stars yajifua Afrika Kusini

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Nov 2018
Stars yajifua Afrika Kusini
Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo Jumatano imefanya mazoezi asubuhi na jioni kwenye Uwanja wa Celtic Bloemfontein nchini Afrika Kusini kujiandaa na mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu Fainali za AFCON dhidi ya Lesotho utakaofanyika Maseru Novemba 18,2018.

Kikosi cha Stars kimetua jana nchini Afrika Kusini kuweka kambi hiyo maalum ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha timu hiyo inafuzu kwa fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika nchini Cameroon.

Stars inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi L ikiwa imejikusanyia alama tano baada ya kushuka dimbani mara nne.

Uganda inayoongoza kundi L, iko katika nafasi nzuri zaidi ya kufuzu ikiwa na alama 10 wakati Cape Verde iko nafasi ya tatu ikiwa na alama nne.

Lesotho inashika mkia katika msimamo wa kundi L ikiwa na alama mbili.

Tanzania, Lesotho na Cape Verde zinawania nafasi ya pili.

Kama Stars itapata ushindi dhidi ya Lesotho halafu Cape Verde ikafungwa na Uganda basi Stars itafuzu sambamba na Uganda.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’