Mshambuliaji hatari wa Simba, Meddie Kagere, amefunguka na kusema sasa anaona fahari kucheza kwenye kikosi cha timu hiyo kutokana na kusheheni wachezaji wenye vipaji ambao wanamsaidia katika kufunga, huku akiahidi kuendelea kutupia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kagere amesema ubora wa kikosi cha Simba unampa matumaini makubwa kuwa timu hiyo itafanya vizuri kwenye michuano yote itakayopshiriki msimu huu.
Mshambuliaji huyo aliyejiunga na Simba msimu huu akitokea Gor Mahia ya Kenya, alisema wachezaji wenzake wamekuwa wakimrahisishia kazi yake uwanjani kutokana na kujua kazi zao.
"Mimi naamini nitaendelea kufunga hata kwenye michezo ya kimataifa, Simba ina wachezaji wazuri katika kila idara, hili kwangu linanipa mwanga wa kuendelea kufanya vizuri katika michezo yetu ijayo," alisema Kagere na kuongeza:
"Kocha amekuwa na mbinu nyingi, zipo timu zinatukamia, lakini kocha amekuwa akitupa mbinu za kukabiliana nazo, " alisema Kagere.
Mshambuliaji huyo mpaka sasa amefunga mabao saba kwenye ligi akiwa miongoni mwa wachezaji watatu waliofunga mabao mengi mpaka sasa.
Kwa sasa mechi za Ligi Kuu kwa timu za Azam FC, Simba na Yanga zimesimama kupisha majukumu ya timu za Taifa zinazosaka tiketi ya kushiriki fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Cameroon.
Kagere yupo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda, huku mshambuliaji mwenza, Emmanuel Okwi wanayefukuzana kwa kufunga Ligi Kuu Bara wote wakicheka na nyavu mara saba, akiwa na kikosi cha Taifa cha Uganda kinachojiandaa kuikaribisha Cape Verde kuwania kufuzu Afcon.

ADVERTISE HERE