Niyonzima atoswa timu ya Taifa ya Rwanda

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Nov 2018
Niyonzima atoswa timu ya Taifa ya Rwanda
Kiungo wa Simba Haruna Niyonzima hajajumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda kinachojiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON 2019 dhidi ya Afrika ya Kati.

Mchezo huo utapigwa nchini Rwanda Novemba 18.

Niyonzima amekuwa kwenye mgogoro na uongozi wa Simba uliopelekea afanye migomo ya mara kwa mara na hivyo kuondolewa kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa Tanzania Bara.

Wakati Niyonzima akiondolewa kwenye kikosi hicho cha Rwanda, Meddie Kagere kinara wa mabao kwenye kikosi cha Simba ameitwa.

Idadi kubwa ya wachezaji wa Simba wameitwa kwenye timu za mataifa yao kwa ajili ya michuano ya AFCON.

Emmanuel Okwi na Juuko Murshidi wao wameitwa timu ya Taifa ya Uganda, wakati Cleotus Chama 'CCC' yeye ameitwa timu ya Taifa ya Zambia.

Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Shiza Kichuya na John Bocco wao wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' inayotarajiwa kusafiri leo kwenda kuweka kambi nchini Afrika Kusini.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
8h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
11h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’