Tully akubali kushindwa, akiri uchaguzi ulikuwa huru

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Nov 2018
Tully akubali kushindwa, akiri uchaguzi ulikuwa huru
Aliyekuwa Mjumbe wa kamati Tendaji ya Simba, Said Tully amesema wanachama wa klabu hiyo walifanya uamuzi sahihi katika uchaguzi wa jana Jumapili.

Alisema hayo mara baada ya Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Boniface Lyamwike kutangaza washindi katika uchaguzi huo.

Tully wa wenzake watatu waliokuwa katika uongozi uliopita hakuna hata mmoja ambaye alipata nafasi ya kurudi kwa maana ya kushinda.

Wajumbe watatu wengine ambao walikuwa katika uongozi uliopita na hawakurudi ni Iddy Kajuna aliyekuwa kaimu makamu Rais wa Simba.

Wengine Ally Suru na Jasmine Badar ambao wote mbali ya kupigiwa kura hazijatosha na kushinda katika uchaguzi wa jana.

"Nadhani kushindwa kwetu wanne ambao tulikuwa katika uongozi uliopita wala sioni tatizo tutajipanga upya na kuona jinsi gani tunaendelea kutoa mchango wetu ndani ya Simba," alisema.

"Wanachama nadhani wamefanya uamuzi sahihi kwa kuchagua viongozi ambao ni sahihi.

"Mchakato mzima wa uchaguzi kwangu ulikuwa mzuri wa kweli na haki wala haukuwa na shida yoyote," alisema Tully.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Goli la ushindi dhidi ya Fountain Gate; FT : Fountain Gate 0-1 Simba
Goli la ushindi dhidi ya Fountain Gate; FT : Fountain Gate 0-1 Simba
6h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Fountain Gate 1-0 Tanzanite Kwaraa
Simba mwendo mdundo, yaichapa Fountain Gate 1-0 Tanzanite Kwaraa
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
9h ago
READ MORE β†’
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
9h ago
READ MORE β†’
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
13h ago
READ MORE β†’
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
13h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’