Mabadiliko Simba yavuta wachezaji 'wakali' Msimbazi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Nov 2018
Mabadiliko Simba yavuta wachezaji 'wakali' Msimbazi
Wakati dirisha la usajili Tanzania Bara likitarajiwa kufunguliwa Novemba 15, mwaka huu, imebainika kwamba wachezaji mbalimbali wa kimataifa kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wameomba kusajiliwa katika klabu hiyo inayonolewa na Mbelgiji Patrick Aussems.

Wachezaji hao wameomba kusajiliwa Simba kutokana na klabu hiyo kwa sasa kumwaga fedha za usajili kutokana na uwepo wa mwekezaji wake, Mohammed Dewji.

Akizungumza jana kwenye mkutano mkuu wa klabu hiyo, Kaimu Rais aliyemaliza muda wake, Salim Abdallah β€˜Try Again’ amesema kwamba wamepokea meseji mbalimbali kutoka kwa wachezaji wa kimataifa wakiomba kusajiliwa katika klabu hiyo.

β€œKuna wachezaji mbalimbali ambao wameomba kusajiliwa katika klabu yetu katika kipindi hiki. Nimekuwa nikipokea meseji za wachezaji kutoka sehemu mbalimbali za Afrika wakiomba nafasi ya kusajiliwa ndani ya timu yetu,” alisema Try Again.

Licha ya wachezaji hao kuomba kusajiliwa na Simba klabu hiyo kwa sasa ina wachezaji nane wa kimataifa. Wachezaji hao ni Emmanuel Okwi (Uganda), Claytous Chama (Zambia), Pascal Wawa (Ivory Coast), Meddie Kagere (Rwanda), Nicholaus Gyan (Ghana), Asante Kwasi (Ghana), Juuko Murshid (Uganda) na James Kotei (Ghana).

Wakati huohuo jana Simba walitangaza kutenga kiasi cha milioni 750 kwa ajili ya kufanya usajili kwa ajili ya kukiimarisha kikosi hicho.

Katika hatua nyingine, Try Again amesema kwamba klabu hiyo tayari imekamilika na wanajua watasajili wachezaji gani kwenye dirisha la usajili ambapo usajili huo utasimamiwa na mwekezaji, Mohammed Dewji β€˜Mo’.

Pia klabu hiyo imesajili wachezaji 17 kwenye kikosi cha vijana cha klabu hiyo U20 pamoja na kusajili wachezaji 10 wanaocheza kwenye timu ya taifa ya wanawake kwa ajili ya Simba Queens.

GPL
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Goli la ushindi dhidi ya Fountain Gate; FT : Fountain Gate 0-1 Simba
Goli la ushindi dhidi ya Fountain Gate; FT : Fountain Gate 0-1 Simba
7h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Fountain Gate 1-0 Tanzanite Kwaraa
Simba mwendo mdundo, yaichapa Fountain Gate 1-0 Tanzanite Kwaraa
8h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
11h ago
READ MORE β†’
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
11h ago
READ MORE β†’
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
14h ago
READ MORE β†’
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
15h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’