Kikosi cha Simba kipo mkoani Mbeya kikiendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 10 dhidi ya Prisons Jumamosi, Novemba 18.
Kikosi cha Simba kitaongezewa nguvu na wachezaji walioitwa kuzitumikia timu zao za Taifa ambapo Watanzania wanatarajiwa kutua jijini Mbeya kesho.
Kocha Mkuu wa Simba Joseph Omog amedhamiria kuondoka na alama zote sita jijini Mbeya baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City.
Simba imekuwa ikipata wakati mgumu inapopambana na Prisons kwenye dimba lao la Sokoine, mwiko ambao Omog ameahidi kuuvunja Jumamosi ijayo.

ADVERTISE HERE