Kaheza, Mo Rashid watemwa kikosi cha Simba CAF

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Nov 2018
Kaheza, Mo Rashid watemwa kikosi cha Simba CAF
Kocha wa Simba Patrick Aussems amewatema washambuliaji Mohamed Rashid na Marcel Kaheza katika kikosi chake kitakachoshiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika yatakayoanza hivi karibuni.

Simba imepata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo ikiwa ni mara ya kwanza baada ya miaka mitano iliyopita.

Viongozi wa Simba walikabidhiwa majina ya wachezaji hao na kocha mkuu Mbelgiji Aussems wamethibisha kuwaacha wawili hao kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.

Wachezaji wengine ambao majina yao yamepelekwa CAF ni Aishi Manula, Deogratius Munishi, Mohamed Hussein, shomary kapombe, Erasto Nyoni, Emmanuel Okwi, Meddie Kagere, John Bocco, Pascal Wawa, James Kotei, Hassan Dilunga, Said Ndemla, Clatous Chama, Juuko Muurshid, Mzamiru Yassin, Shiza Kichuya, Adam Salamba na Haruna Niyonzima.

Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah 'Try Again' alikiri kupeleka kikosi chao TFF na kwamba hivi karibuni watatangaza wachezaji watakaiwakilisha Simba na wale watakaobaki ikiwa ni pamoja na sababu za kuwaacha.

"Tulipeleka majina muda mrefu bado kuyatangaza tu, ila tutayatangaza hivi karibuni," alisema Try Again ambaye hakuwa tayari kuweka wazi walioachwa na wale watakaoingia kwenye vita hiyo ya kimataifa.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’