Simba yawanyemelea Mastraika wawili

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Nov 2017
Simba yawanyemelea Mastraika wawili
Simba inawanyemelea wachezaji wa kigeni kutoka Rwanda anakotokea kiungo mahiri, Haruna Niyonzima.

Wa Kwanza ni kiraka Muhire Kelvin ambaye ana uwezo zaidi wa kucheza namba kumi ameng'ara na klabu ya Isonga, akaibukia Rayon Sport na baadaye Shakhtyor Soligorsk ya Belarus.

Muhire alizaliwa Oktoba 17, 1998 na amecheza timu ya Taifa ya vijana ya Rwanda chini ya miaka 23.

Kifaa kingine ambacho Simba wanakiwinda ni Shasir Nahimana mwenye uwezo mkubwa wa kufunga na amekuwa moja ya wachezaji nyota kwenye Ligi Kuu Rwanda akiichezea Rayon Sport.

Nahimana ambaye amezaliwa Agosti, 1993 anavaa jezi namba kumi na huenda Simba walimuona katika mechi ya kirafiki ambayo walicheza Dar es Salaam Simba Day, lakini kama haitoshi aliwafunga Azam bao moja kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa Rwanda Julai 8, 2017.

Mmoja wa viongozi wa Simba amesema kwamba Kocha Msaidizi, Masoud Djuma, amewahakikishia wachezaji hao wana uwezo kuliko baadhi ya mastaa wa kigeni walioko Simba kwa sasa.

Ujio wa wachezaji hao unaamaanisha wakisajiliwa basi wachezaji wawili wa kigeni wataenda na maji Msimbazi huku Mghana, Nicolaus Gyan na Mrundi, Laudit Mavugo wakitajwa.

Mavugo anatajwa kujiunga na Gor Mahia ya Kenya na huenda akaondoka hata kabla ya maandalizi ya Krismasi hayajaanza kama mambo yatakwenda sawa.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
12h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
15h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’