Mkutano Mkuu wa Wanachama wa klabu ya Simba unatarajiwa kufanyika Jumapili Novemba 04 ukienda sambamba na uchaguzi wa viongozi wa Simba utakaofanyika Novemba 05.
Afisa Habari wa Simba Haji Manara amewataka wanachama wa klabu hiyo kuchagua viongozi ambao wataipa mafanikio Simba.
"Twendeni tukachague Viongozi ambao hatuna shaka nao juu ya Mustakbali wa Muundo mpya wa Simba", Manara amewaambia waandishi wa habari leo.
"Tuchague viongozi ambao wataipeleka Simba mbele zaidi,Viongozi wanaojua nini mahitaji ya sasa ya klabu
"Linapokuja swala la uchaguzi kipaumbele chetu kiwe Simba SC, tusisahau pia Viongozi tutakaowachagua ni Wawakilishi wa Wanachama kwenye Bodi ya Wakurugenzi hivyo ni lazima wawe watu Weledi na Wajuzi wa mambo"

ADVERTISE HERE