TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Klabu ya Simba leo Alhamisi tarehe 1/11/2018 Saa Sita Mchana, kwenye Makao Makuu yake Mtaa wa Msimbazi hapa jijini, itazungumza na waandishi wa habari.
Mkutano huo unalenga kuuhabarisha umma, pamoja na mambo mengine juu ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa klabu na ule wa Uchaguzi, mikutano yote hiyo inatarajiwa kufanyika siku ya Jumapili ijayo ya Tarehe 4/11/2018 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) uliopo Maeneo ya Ocean Road hapa Dar es Salaam.
Kama ilivyo desturi Mkutano wa kesho na wanahabari, utarushwa mubashara (Live) na kituo maarufu nchini cha Azam TV kupitia chaneli yake ya Azam Sports Two, sambamba na kurasa za mitandao ya kijamii ya klabu na za Msemaji wa Mabingwa hao wa Nchi.
Imetolewa na
Haji S Manara
Mkuu wa Habari na Mawasiliano
Simba SC
SIMBA NGUVU MOJA

ADVERTISE HERE