Kocha mkuu wa Simba, Mcameroon Joseph Omog amewahakikishia mambo mazuri mashabiki wa timu hiyo baada ya kufanya marekebisho ndani ya kikosi chake na akasema, jukumu la ulinzi ni la wachezaji wote.
Omog amesema, ndani ya kipindi hicho ambacho walicheza pia mchezo wa kirafiki na Milambo ya Tabora wakamaliza kwa suluhu ya bila kufungana.
Omog amesema: "Kama nilivyosema, timu ilikuwa na mapungufu katika umakini na ndiyo kilitusababishia hata tukapata matokeo yale, tukaruhusu mabao ya kufungwa, lakini sasa kila kitu kinakwenda sawa."
"Suala la ulinzi ni la wachezaji wote ndivyo nataka timu icheze, kama ni ushambuliaji pia ni kwa wote ndiyo mafanikio ya Simba hakuna wa kulaumiwa ndiyo maana ikaitwa timu," alisema Omog.
Simba ipo Kanda ya Ziwa ikiendelea na maandalizi yake, inajiandaa na mchezo wake dhidi ya Stand United utakaochezwa Shinyanga wikiendi hii.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE