Gari imekata breki! Ndio kauli unayoweza kuitumia kwa kiwango kinacho onyeshwa na mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba baada ya leo kuwafumua Ruvu Shooting mabao 5-0 kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa.
Ushindi huo mnono unaifanya Simba iwe imefunga mabao 10 kwenye michezo miwili. Jumatano iliyopita iliifumua Alliance mabao 5-1!
Ilikuwa ni jioni mbaya sana kwa msemaji wa Ruvu Shootinga Masau Bwire ambaye kauli zake zinaweza kuwa zimeiponza timu yake siku ya leo
Emmanuel Okwi ameendeleza rekodi yake ya kupachika mabao dhidi ya Ruvu Shooting leo akifunga hat-trik yake ya kwanza msimu huu.
Msimu uliopita katika ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya maafande hao, Okwi alipachika mabao manne.

Meddie Kagere na Adam Salamba nao walifanikiwa kuzifumania nyavu na kuihakikishia Simba ushindi muhimu.

Makali ya kocha Patrick Aussems yameanza kuzipa wakati mgumu timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu ya Tanzania Bara.
Washambuliaji wa Simba wameongeza umakini na wameanza kuzitumia ipasavyo nafasi wanazotengeneza.
Kwa hakika kauli ya kocha wa timu ya vijana ya Simba Mussa Mgosi kuwa kuna siku itashuhudiwa timu ikifungwa mabao 10 na Simba kwenye dimba la Taifa inaweza kutimia.
Matokeo ya michezo yote iliyopigwa leo

ADVERTISE HERE