Simba kuikabili Ruvu Shooting uwanja wa Taifa leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Oct 2018
Simba kuikabili Ruvu Shooting uwanja wa Taifa leo
Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba leo wanashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara raundi ya 12.

Ruvu Shooting itakuwa mwenyeji wa mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa moja usiku.

Wakati Simba ikiendelea na maandalizi yake kimyakimya, tambo nyingi zimesikika kutoka kwa msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire.

Baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Singida United kwenye mchezo uliopita, Bwire anadai leo wataendeleza wimbi la ushindi uwanja wa Taifa.

Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika. Wataingia uwanja wa Taifa kuivaa Ruvu Shooting wakiwa na lengo la kuondoka na alama zote tatu.

Manara amesema wanafahamu Ruvu Shooting imepania mchezo huo lakini wao hawana wasiwasi kwani timu zote zinazocheza na Simba zina kawaida ya kupania lakini baada ya dakika 90 wanaondoka vichwa chini.

"Kikosi chetu kiko tayari kwa mchezo huo. Tunafahamu hautakuwa mchezo mwepesi lakini tuna imani tutaondoka na alama zote tatu," Manara aliiambia Azam TV.

Msimu uliopita Ruvu Shooting ilifungwa jumla ya mabao 10 na Simba ambapo mzunguuko wa kwanza ilikula bao 7-0 huku mzunguuko wa pili ikirambishwa mabao 3-0
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
13h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
17h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’