Kiraka Erasto Nyoni na kiungo James Kotei raia wa Ghana wataukosa mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kesho Jumapili.
Lakini habari njema ni kurejea kikosini kwa kiungo Jonas Mkude aliyekuwa nje kwa zaidi ya wiki mbili akisumbuliwa na majeraha ya goti.
Nyoni na Kotei wanakosa mchezo huo kwa sababu ya adhabu wanazotumia kutokana na makosa mbalimbali waliyofanya.
Nyoni alimpiga kiwiko, Hassan Nassoro Maulid wa Ndanda SC katika mchezo wao waliosuluhu Uwanja wa Nangwanda, Sijaona.
Kotei, alikutana na adhabu hiyo kwa kosa la kumpiga ngumi, Gadiel Michael wa Yanga katika mechi iliyowakutanisha wakongwe hao wa Ligi Kuu Bara
Wekundu wa Msimbazi wamepania kuzima ngebe za msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire ambaye amekuwa akitamba kwenye vyombo vya habari kuwa timu yake itaibuka na ushindi kwenye mchezo huo

ADVERTISE HERE