Aussems atamba, moto wa mabao hauzimi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Oct 2018
Aussems atamba, moto wa mabao hauzimi
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems anawashangaa mashabiki wa soka ambao wanahoji juu ya kikosi chake kufunga mabao mengi wakati zamani walimponda kwa kukosa mabao.

Aussems ambaye kwa sasa kikosi chake ndiyo vinara wa mabao Ligi Kuu Bara wakiwa wamefunga 16, Yanga ya pili ina 15 na Azam FC wakiwa watatu na mabao 13.

"Mwanzo mlisema hatufungi mabao mengi lakini sasa mnasema tunafunga sana. Unajua mwanzo tulikuwa hatufungi lakini tulikuwa tunatengeneza nafasi nyingi za mabao,"alisema Aussems.

Amefafanua, kilichowafanya wachezaji wake wabalike ni majaribio waliyokuwa wanafanya katika mazoezi yao ambayo ndani ya wiki mbili hadi tatu yameleta majibu.

Simba ndiyo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, hawakuanza vizuri katika mechi za mwanzoni mwa msimu lakini sasa wanashika nafasi ya tatu na pointi 20, Azam ndiyo vinara wakiongoza na pointi 24 huku Yanga ikiwa ya pili na alama 22.

Azam imeshuka dimbani mara 10 wakati Simba na Yanga zimecheza michezo pungufu, Simba imecheza michezo tisa na Yanga michezo nane.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’