Chama amkuna Hans Poppe

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Oct 2018
Chama amkuna Hans Poppe
Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Simba Zacharia Hans Poppe ndiye aliyefanikisha usajili wa Mzambia Clateous Chama ambaye kiwango chake kimeendelea kuwaduwaza wengi.

Juzi Hans Poppe alikuwepo uwanja wa Taifa kumshuhudia kiungo huyo katika mchezo dhidi ya Allance.

Chama aliifungia Simba bao la tano kwenye dakika ya 87 kukamilisha ushindi wa mabao 5-1.

Bao hilo lilimsisimua Hans Poppe aliyekuwa ameketi sambamba na viongozi waandamizi wa klabu ya Simba wakiongozwa na Kaimu Rais Salim Abdallah 'Try Again'

Usajili wa Chama pamoja na ule wa Meddie Kagere unatajwa kuwa usajili bora zaidi kufanywa na Simba msimu huu.

Wawili hao wamekuwa na msaada mkubwa kwenye kikosi cha Simba.

Kagere amefunga mabao manne wakati Chama amefunga mabao mawili huku akiwa ndio 'engine' ya Simba katika kutengeneza mashambulizi
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
48m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’