Ajib bado hajakamilika kuitumikia Stars - Amunike

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Oct 2018
Ajib bado hajakamilika kuitumikia Stars - Amunike
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Stars, Emmanuel Amunike ameweka wazi kwa kusema kuwa hawezi kumuita mchezaji yeyote ndani ya timu ambaye hajakamilika akiwemo Ibrahim Ajibu ila akiona anafaa anaweza kumuita.

Ajibu amekuwa akifanya vizuri ndani ya timu ya Yanga na kutoa mchango mkubwa Ligi Kuu Bara baada ya kuhusika kwenye mabao 11 kati ya 15 waliyofunga ila hajaitwa timu ya Taifa.

Ammunike amesema kuwa watu wanapaswa watambue kucheza timu ya taifa ni jambo lenye maana kubwa kwa mchezaji hivyo siyo kila mchezaji anaweza kuitwa kwa kuwa ni msaada kwenye klabu yake.

β€œYapo mambo mengi ambayo yanazingatia mchezaji kuitwa timu ya taifa, mchezaji anatakiwa awe amekamilika na kujua nchi inataka nini na siyo kila mchezaji anayefanya vizuri anaitwa timu ya taifa, maana klabu na timu ya taifa ni vitu viwili tofauti, sisemi kwamba hatacheza ila nitakapoona anafaa naweza kumuita,” alisema Amunike.

Stars inatarajiwa kuweka kambi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Lesotho kwa ajili a Kufuzu Fainali za Michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) Cameroon
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
44m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’