FT : Simba 5-1 Alliance

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Oct 2018
FT : Simba 5-1 Alliance
Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba leo wameiadhibu vikali Alliance Fc kutoka jijini Mwanza kwa kuifumua mabao 5-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa.

Ubora wa kikosi cha Simba ulizima kabisa vijana wa Alliance na kujikuta wanaondoka dimba la Taifa wakiwa na kapu lililojaa mabao ya wekundu wa Msimbazi



Simba ilijipatia mabao yake kupitia kwa Emmanuel Okwi aliyepachika mabao mawili, Asante Kwasa, Adam Salamba na Mzambia Cleotus Chama ambaye ameendeleza kuwashangaza wengi kutokana na uwezo mkubwa anauonyesha dimbani.

Bao pekee la kufutia machozi kwa upande wa Allince lilipatikana kwenye dakika za majeruhi likiwekwa kambani na Zabona Khamisi.





Mganda Emmanuel Okwi amerejesha makali yake ya kuzifumania nyavu kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo mabao yake mawili ya leo yamemfanya afikishe mabao manne sasa akiwa sawa na Meddie Kagere

Ushindi huo umeipeleka Simba hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 20.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’