Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba leo kimefanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Boko Veterans jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Allince Fc kesho Jumatano.
Simba itakuwa mwenyeji wa mchezo huo utakaopigwa uwanja wa taifa ukitarajiwa kuanza saa moja usiku.
Simba imejifua ikiwa na kikosi chake kamili kilichowajumuisha nahodha John Bocco aliyemaliza adhabu ya kufungiwa michezo mitatu na Jonas Mkude aliyekosa mchezo dhidi ya Stand United kutokana na majeruhi.
Mazoezi hayo yalisimamiwa kikamilifu na kocha Patrick Aussems ambaye amesema wana matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi mnono kwenye mchezo huo

ADVERTISE HERE