Bao lililokataliwa la kiungo mshambuliaji wa Simba, Mohammed Ibrahim dhidi ya Stand United juzi, limemponza mwamuzi msaidizi, Haji Mwarukuta kutoka Tanga ambaye ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi.
Mwarukuta alikataa bao hilo lililofungwa dakika ya 50 akidai Ibrahim aliotea kabla ya kufunga, baada ya kuwahi mpira uliogonga mwamba na kurudi uliotokana na shuti la faulo iliyopigwa na Said Ndemla, lakini kiuhalisia, kiungo huyo mshambuliaji wa Simba hakuwa ameotea.
Kukataliwa kwa bao hilo kumeibua mjadala miongoni mwa kundi kubwa la wadau wa soka ambao wengi wameshangazwa na uamuzi huo ambao uliinyima Simba nafasi ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0.
Simba ilishinda mabao 3-0, katika mchezo huo yaliyofungwa na Cletus Chama, Emmanuel Okwi na Meddei Kagere.
Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Salum Chama alisema wamemchukulia hatua mwamuzi huyo msaidizi kwa kushindwa kutafsiri sheria ya kuotea.
"Nadhani tatizo siyo TFF au Bodi ya Ligi ni waamuzi wenyewe, ukiangalia lile bao wala haihitaji kazi ngumu kubaini lilikuwa ni halali lakini sijajua refa alifikiria nini hadi akakataa.<
“Tumeshakutana kama kamati na kujiridhisha kuwa mwamuzi msaidizi alifanya makosa, hivyo tumemchukulia hatua kwa kumuondoa kwenye orodha ya waamuzi na tunatoa angalizo tutaendelea kuchukua hatua kwa waamuzi wote watakaochezesha chini ya kiwango," alionya Chama.

ADVERTISE HERE