Okwi, Kichuya watakiwa Ubelgiji

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Oct 2018
Okwi, Kichuya watakiwa Ubelgiji
Baada ya kuibuka kwa taarifa kwamba wachezaji wawili wa Simba Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya kutakiwa na klabu moja nchini Ubelgiji, uongozi wa Simba umezialika mezani timu zinazowataka wachezaji hao.

Akizungumza kuhusu mustakabali wa wachezaji hao, Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema klabu hiyo haina utamaduni wa kuzuia wachezaji wanapopata timu nje ya nchi.

"Timu yoyote inayotaka mchezaji wetu ije mezani tuzungumze. Kama tutafikia makubaliano basi hatuna tatizo," amesema Manara.

"Mchezaji akipata timu huko nje ni faida kwake, kwa timu yake ya Taifa na kwetu pia kwani tunapata fedha za kigeni"

Kichuya bado ana mkataba wa muda mrefu na Simba baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili mwanzoni mwa msimu.

Mkataba wa Okwi unamalizika mwishoni mwa msimu. Lakini uongozi wa Simba una mpango wa kufanya nae mazungumzo ya mkataba mpya.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Goli la ushindi dhidi ya Fountain Gate; FT : Fountain Gate 0-1 Simba
Goli la ushindi dhidi ya Fountain Gate; FT : Fountain Gate 0-1 Simba
5h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Fountain Gate 1-0 Tanzanite Kwaraa
Simba mwendo mdundo, yaichapa Fountain Gate 1-0 Tanzanite Kwaraa
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
9h ago
READ MORE β†’
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
9h ago
READ MORE β†’
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
12h ago
READ MORE β†’
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
12h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’