Kocha Mkuu wa Simba Joseph Omog amesema kikosi chake kina maoungufu machache hivyo pengine atasajili wachezaji wawili tu kwenye dirisha dogo la usajili linalofunguliwa keshokutwa Jumatano.
Simba inaongoza ligi ikiwa na alama 19 sawa na Azam FC lakini imefunga mabao mengi zaidi.
Omog amesema timu yake ina mapungufu upande wa ulinzi wa kulia pamoja na mshambuliaji wa kati.
Shomari Kapombe aliyesajiliwa kwa ajili ya ulinzi wa kulia ameshindwa kuvaa uzi wa Simba hata kwenye mchezo wa kirafiki kutokana na majeraha ya muda mrefu.
Huenda Simba ikavunja mkataba wake kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.
Omog pia ameona ni muhimu kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji baada ya washambuliaji waliopo kushindwa kuifanya kazi yao.
Mabao mengi ya Simba yamefungwa na viungo.
Omog amedhamiria kuisaidia Simba kutwaa ubingwa wa VPL msimu huu baada ya 'kuukosakosa' msimu uliopita kwa kuzidiwa mabao na Yanga.

ADVERTISE HERE