Ninje aula TFF

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Oct 2018
Ninje aula TFF
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) iliyokutana Jumamosi Oktoba 20,2018 Makao Makuu ya TFF Karume,Ilala ilipitia masuala mbalimbali ikiwemo kumthibitisha Ammy Ninje kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF.

Ninje aliyewahi kuinoa timu ya Taifa ya Tanzania Bara kwenye michunao ya Chalenji mwaka uliopita, amechukua nafasi ya Salum Madadi ambaye amebadilishiwa majukumu.

Kamati hiyo pia ilipitia masuala mbalimbali ikiwemo kuchagua wajumbe wa kamati ya Uchaguzi, Kamati ya Nidhamu na Rufaa Maadili.

Pia Kamati ya Utendaji imepitisha tarehe ya Mkutano Mkuu wa TFF wa mwaka utafanyika Jijini Arusha Disemba 29,2018

Mkutano huo unafanyika kwa mujibu wa Katiba ya TFF na umepata siku 60 za kutangazwa kabla ya kufanyika

Aidha kikao hicho cha Kamati ya Utendaji kimepitisha mabadiliko madogo kwenye kamati ndogo ndogo za TFF.

Mabadiliko hayo yametokana na baadhi ya Wajumbe kujiuzulu na Wajumbe wengine kukabiliwa na majukumu mengi.

KAMATI YA UCHAGUZI

1.MALANGWE ALLY -Mwenyekiti
Mh. MOHAMED MCHENGELA -M/Kiti

3.BENJAMINI KARUME - Mjumbe
4.MOHAMED GOMBATI - Mjumbe
5.HAMISI ZAYUMBA - Mjumbe

KAMATI YA NIDHAMU

1.KIOMONI KIBAMBA - Mwenyekiti
2.PETER HELLA - M/Mkiti
3.KASSIM DAU - Mjumbe
4.HANDLEY MATWENGA - Mjumbe
5.TWAHA MTENGERA - Mjumbe

KAMATI YA RUFAA MAADILI

1.RICHARD MBARUKU - Mwenyekiti
2.THADEUS KARUA -M/Kiti
3.MH . MUSSA ZUNGU -Mjumbe
4.ASP BENEDICT NYAGABONA-Mjumbe
5.LUGANO HOSEA -Mjumbe
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
5h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
11h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
14h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’