Mzambia Cleoteus Chama jana aliwakosha mashabiki wa klabu ya Simba kwenye mchezo dhidi ya Stand United ambapo alipachika moja ya mabao.
Tangu ajiunge na Simba mwanzoni mwa msimu Chama ameonyesha kiwango cha hali ya juu kiasi ambapo viongozi wa Simba wamepongezwa kwa kufanikisha usajili wake.
Jana baada ya mchezo baadhi ya mashabiki walimtuza fedha Mzambia huyo ambaye pia ni mchezaji wa kutegemewa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Zambia, Chipolopolo.
Mmoja wa watu walioguswa na uwezo wa Chama ni Afisa habari wa Simba Haji Manara ambaye amesema kiungo huyo katika mchezo wa jana alimsahaulisha machungu ya kulala 'sero'
"Clateous Chama Mwamba wa Lusaka amenifanya nisahau machungu yote niliyokuwa nayo polisi , pongezi sana kwa Mwenyekiti kamati ya usajili simba sc nitamrejeshea nauli yake aliyetumia kwenda Lusaka kuleta chuma hiki"

ADVERTISE HERE