Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba Zacharia Hans Poppe jana alikuwa mkoani Iringa ambapo alishuhudia mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya Lipuli Fc dhidi ya Kagera Sugar.
Baada ya mchezo huo ambao Lipuli ilifungwa bao 1-0, Hans Poppe aliichangia timu hiyo fedha taslimu Tsh Milioni mbili kuisaidia klabu hiyo kusafiri kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo dhidi ya Mbao Fc.
Hivi karibuni Hans Poppe aliachiwa kwa dhamana katika kesi inayomkabili ya kutoa taarifa za uongo kwa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA)
Alifikishwa Mahakamani wiki iliyopita siku moja baada ya kuwasili kutoka nchini Marekani alikokuwa amekwenda kwa ajili ya matibabu.

ADVERTISE HERE