Mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi leo amefunga bao lake la pili kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara msimu huu alipoiongoza Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Stand United.
Akizungumza baada ya mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa, Okwi amesema ushindi mnono uliopatikana leo ni ishara kwamba safu yao ya ushambuliaji imeanza kuelewana.
"Kuna nafasi nyingi mbele tunazipata ila hatuzitumii vizuri ila nashukuru Mungu tumeanza kuelewana naamini tutafunga magoli mengi zaidi," amesema Okwi.
Aidha Okwi amesema wameufanya ushindi huu kuwa mahsusi kwa ajili ya mlezi na Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji aliyekuwa ameshikiliwa mateka na watu wasiojulikana kwa siku kumi kabla ya kuachiwa usiku wa kuamkia jana.
"Ushindi huu ni Zawadi kwa Mwekezaji wetu aliyepata matatizo Mohammed Dewji 'MO' tunampa pole sana na tunamkaribisha tena kwenye timu yetu"

ADVERTISE HERE