Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo wametakata uwanja wa Taifa baada ya kuifumia Stand United mabao 3-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
Licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji wake waandamizi Erasto Nyoni, Jonas Mkude na John Bocco, Simba ilionyesha kandanda safi na ushindi huo haukuwa na shaka.
Simba iliuanza mchezo huo kwa kasi na ilikosa mabao kadhaa ya wazi kabla ya Cleouts Chama kuitanguliza kwenye dakika ya 31 akifunga bao safi kwa shuti kutoka winga ya kushoto.
Mganda Emmanuel Okwi akaiongezea Simba bao la pili kwenye dakika za majeruhi kipindi cha kwanza akimalizia shambulizi la kushitukiza lililoanzishwa na Chama.

Bao la tatu la Simba lilipatikana kwenye dakika ya 78 baada ya mpira wa kona uliochongwa na Shiza Kichuya kutua kichwani kwa mlinzi wa Stand United Eric Mlilo aliyeujza mpira kimiani.
Ushindi wa leo umeipeleka Simba hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 17 ikizipiku Singida United, Mtibwa Sugar, JKT na Mbao kwa wingi wa mabao
Aidha ushindi huo ni zawadi mahsusi kwa mlezi na Mwekezaji wa Simba Mohammed Dewji ambaye alikumbwa na matatizo ya kutekwa na watu wasiojulikana kabla ya kuachiwa usiku wa kuamkia jana.

ADVERTISE HERE