Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba jioni ya leo wanashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Stand United katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara mzunguuko wa 10.
Kikosi cha Simba ambacho kilipata msukosuko baada ya kutekwa kwa mlezi na mwekezaji wake Mohammed Dewji 'MO', kiko kamili na tayari kwa mchezo huo huku mzuka ukiwa umeongezeka mara dufu baada ya kupatikana kwa MO hapo jana.
Huenda MO akaibuka uwanja wa Taifa leo kuushuhudia mchezo huo pia kutoa shukrani kwa mashabiki wa Simba na Watanzania wote ambao hawakuchoka kumuombea wakati wote aliokuwa anashikiliwa mateka na watu wasiojulikana.
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema vijana wake wana ari kubwa kuelekea mchezo huo na ana imani wataibuka na ushindi mnono leo.
Ushindi katika mchezo huu itakuwa zawadi mahsusi kwa MO lakini pia utanogesha furaha ya Wekundu wa Msimbazi.

ADVERTISE HERE