Michezo minne TPL yapigwa leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Oct 2018
Michezo minne TPL yapigwa leo
Ligi Kuu ya Tanzania Bara imeendelea leo Jumamosi kwa michezo minne kupigwa katika viwanja mbalimbali.

Mchezo wa mapema uliishuhudia Tanzania Prisons ikitoshana nguvu na Singida United baada ya kutoka suluhu bila ya kufungana.

Coastal Union nayo imetoka suluhu bila ya kufungana dhidi ya JKT Tanzania huku Biashara United nayo ikitoka suluhu ya bila ya kufungana dhidi ya KMC.

Yanga ndio timu pekee iliyopata ushindi katika michezo ya leo baada ya kuilaza Alliance Fc mabao 3-0 kwenye mchezo uliopigwa dimba la Taifa.




Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Simba wao wanashuka dimba la Taifa kesho Jumapili kuikabili Stand United katika mchezo ulio na sifa ya kipekee.

Ushindi katika mchezo huo itakuwa ni zawadi mahsusi kwa mwekezaji wa Simba Mohammed Dewji 'MO' ambaye baada ya kushikiliwa mateka na watu wasiojulikana kwa siku 10, usiku wa kuamkia leo aliachiwa.

Mashabiki wa klabu ya Simba wametakiwa wajitokeze kwa wingi kwenye uwanja wa Taifa kuonyesha umoja na mshikamano wao hasa baada ya kipindi kigumu cha kutekwa mwekezaji wao
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
9h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
15h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’