Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limeiruhusu klabu ya JKT Tanzania kutumia uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga kwa ajili ya michezo yake dhidi ya Simba na Yanga.
TFF imeiruhusu timu hiyo kupeleka michezo yake jijini Tanga dhidi ya vigogo hao wa soka nchini kutokana na uwanja wake wa nyumbani inaotumia sasa wa Meja Jenerali Isamuhyo ulioko Mbweni Dar es Salaam, kutokuwa na uwezo wa kuhimili wingi wa mashabiki wa timu hizo.
Kutokana na mabadiliko hayo, mchezo kati JKT Tanzania dhidi ya Simba ambao awali ulipangwa kupigwa uwanja wa Taifa, Novemba 03 sasa utapigwa dimba la Mkwakwani.
Yanga nayo itasafiri kwenda mkoani humo kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya JKT Tanzania ambao awali ulipangwa kupigwa Septemba 26 lakini ukaahirishwa kutokana na mpambano wa watani wa jadi.

ADVERTISE HERE