Baada ya mapumziko ya siku 10 kupisha michezo ya Kimataifa, ligi kuu ya Tanzania Bara inarejea rasmi leo kwa michezo mitatu kupigwa.
Ndanda Fc ambayo mapema wiki hii iliomba michango ya wadau wake ili ipate nauli ya kuiwezesha kurudi Mtwara baada ya kukwama mkoani Singida, itashuka kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona kuikabili Mbeya City.
Mwadui Fc itacheza na Ruvu Shooting mkoani Shinyanga wakati Azam FC itakuwa kwenye dimba lake ya Azam Complex, Chamazi kupepetana na African Lyon katika mchezo utakaopigwa saa moja jioni.
Ligi hiyo itaendelea Jumamosi kwa michezo mingine mitatu kupigwa huku mabingwa watetezi Simba wakitarajiwa kushuka dimbani keshokutwa Jumapili kuikabili Stand United kwenye mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Taifa.
Hii hapa ratiba ya michezo yote ya wikiendi hii;

ADVERTISE HERE