Leo zimetimia siku saba tangu Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji atekwe na watu wasiojulikana.
Wiki hii imekuwa ngumu sana kwa familia ya klabu ya Simba na tasnia ya soka nchini kwa ujumla.
Kutekwa kwa MO kumeibua taharuki miongoni mwa Wana Msimbazi na tukio hilo limewaumiza mashabiki, viongozi na wachezaji wa Simba.
Kwa nyakati tofauti benchi la Ufundi lililazimika kuahirisha mazoezi ili kuwapa nafasi wachezaji watulize akili na kushiriki katika ibada maalum za kumuombea MO.
Lakini tangu Jumatatu, Simba imekuwa ikijifua kikamilifu kwenye uwanja wa Boko Veterans kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Stand United utakaopigwa Jumapili, Oktoba 21 kwenye uwanja wa Taifa.
Wachezaji wa Simba wameahidi kuwa watahakikisha wanashinda mchezo huo ili ushindi uwe faraja kwa Wana Msimbazi wote katika kipindi hiki kigumu.
βMechi yetu na Stand ni muhimu kuliko hata zile tulizocheza tangu ligi ianze," alizungumza Shiza Kuchuya, kiungo wa Simba
"Tunahitaji kurejesha furaha kwenye nyuso za mashabiki wetu hasa katika kipindi hiki kigumu tunachopitia kutokana na tukio lililomkumba kiongozi wetu"

ADVERTISE HERE