Ujenzi uwanja wa Simba unaendelea Bunju, utakamilika Februari 2019

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Oct 2018
Ujenzi uwanja wa Simba unaendelea Bunju, utakamilika Februari 2019
Uwanja mpya wa Klabu ya Simba unaojengwa katika eneo la Bunju jijini Dar es Salaam, unatarajiwa kumalizika ifikapo Februari mwakani imefahamika.

Ujenzi huo unaendelea kama kawaida licha ya kutekwa kwa mwekezaji na mwanachama wa klabu hiyo, Mohammed Dewji 'MO' ambaye ndiye anatoa fedha za kuendesha mradi huo.<

Msimamizi wa ujenzi huo, Danny Matiku, amesema kazi ya ujenzi huo inaendelea kwa kasi kama ilivyopangwa na wanaamini wataikamilisha katika muda uliopangwa.

Matiku alisema kwa sasa tayari wameshamaliza kazi ya kumwagia kifusi na tayari wameanza kuweka mabomba ambayo yatapitishia maji ili mvua itakaponyesha, yasiweze kutuama kwenye eneo la kuchezea.

Msimamizi huyo alisema uwanja huo utakuwa ni wa nyasi bandia na kwa sasa pia wameshakamilisha uzio ambao unawatenganisha wachezaji na mashabiki watakaokuja uwanjani hapo.

"Ujenzi unaendelea kama kawaida kwa sababu hii ni kazi ambayo iko kwenye mkataba, uwanja utakuwa na viwango vinavyotakiwa, tayari tumeshakamilisha kumwaga vifusi na zoezi linalofuata katika eneo hili la kuchezea kutandika nyasi bandia, ukuta wa kubeba uwanja umeshakamilika na huku pembeni tutaweka vyuma," alisema msimamizi huyo.

Aliongeza kuwa baadaye watawakaribisha maofisa kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) ili kukamilisha vipimo rasmi ambavyo vinaruhusiwa na shirikisho hilo.

IPP Media
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’