Afisa Habari wa Simba Haji Manara amewataka Watanzania wasichoke kumuombea Mfanyabishara na Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji 'MO' ambaye leo imetimia wiki moja tangu alipotekwa na watu wasiojulikana.
Manara ambaye alishikiliwa na jeshi la Polisi kusaidia upelelezi wa tukio hilo kabla ya kuachiwa kwa dhamana mapema wiki hii, amesema tukio la kutekwa MO ndio baya zaidi alilowahi kukutana nalo tangu awe kiongozi wa Simba.
"Wiki moja kamili imetimia toka tukio la kutekwa kwa kiongozi wetu MO litokee," Manara ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
"Kwangu mimi binafsi ni tukio baya sana toka nimeanza kazi Simba na Moyo wangu bado umesinyaa
"Tuendelee kumuomba Mola apatikane akiwa Mzima na salama, faraja pekee ninayopata ni kuona Watanzania walio wengi tumeungana kumtakia kheri kipngozi wetu,
"Naamini Dua na Sala zetu zitasikika na Insha'Allah kwa jitihada za vyombo vyetu na matakwa yake Mwenyezi,mambo yatakaa sawa"

ADVERTISE HERE