Simba yaiwinda Stand United

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Oct 2018
Simba yaiwinda Stand United
Kikosi cha mabingwa wa Tanzania Bara, Simba kimeendelea kujifua kwenye uwanja wa Boko Veterans jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Stand United.

Mchezo huo utapigwa Jumapili, Oktoba 21 kwenye uwanja wa Taifa.

Baadhi ya wachezaji waliokuwa wamekwenda kuzitumikia timu za Taifa wameanza kuwasili kikosini kuendelea na program za kocha Patrick Aussems.

Mshambuliaji Meddie Kagere aliyekuwa amekwenda Rwanda kuitumikia timu Taifa hilo amekuwa miongoni mwa wachezaji waliorejea mapema baada ya kuwasili leo.

Wachezaji wengine wanaotarajiwa kuwasili mapema kabla ya mchezo wa Jumapili ni Juuko Murshidi na Emmanuel Okwi (Uganda), Haruna Niyonzima (Rwanda) na Cletus chama (Zambia).

Aidha nahodha John Bocco, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni na Aishi Manula waliokuwa timu ya Taifa ya Tanzania wao wanatarajiwa kuanza mazoezi kesho baada ya kupewa mapumziko ya siku moja.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
7h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
13h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
16h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’